Everyone has a story!

Share your story with the world

Vitendo Bilioni 7

Harakati ya Kimataifa kwa ajili ya watu wote

Idadi ya watu duniani itafikia watu bilioni 7 tarehe 31 Oktoba, 2011. Wakati huu wa kipekee katika historia ya mwanadamu unawakilisha mafanikio na changamoto, na utakuwa na athari kwetu sote. Dunia ya watu bilioni saba itakuwa na taathira kwa uendelevu, uanzishwaji wa miji, upatikanaji wa huduma za afya na uwezweshaji wa vijana – hata hivyo, dunia hiyo pia itatoa wito adimu wa kufanya kwa vitendo ili kutimiza ahadi ya kimataifa kwa ajili ya dunia yenye afya na endelevu.

Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa unaongoza kampeni bunifu ya kimataifa – Vitendo bilioni 7. Mpango huo umeitishwa na UNFPA na unamilikiwa na washirika wengi kutoka katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, jamii ya mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi pamoja na wasomi. Mpango huo uko wazi kwa kwa mashirika yote na watu binafsi wenye nia ya kuboresha ulimwengu wa watu bilioni saba.

Tusaidie kuadhimisha tarehe hizi muhimu

• Tarehe ya uzinduzi wa Vitendo bilioni 7: Septemba 14, 2011
• Siku zilizosalia kufikia watu bilioni 7 duniani: Oktoba 24, 2011
• Launch of the State of World Population report: October 26th, 2011
• Uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya Watu Duniani: Oktoba 16, 2011
• Siku ya watu Bilioni 7 duniani: Oktoba 31, 2011
• Baada ya tarehe 31 Oktoba: Mpango huu bunifu utaendelezwa hadi mwaka 2012, huku ukiambatana na matukio mbalimbali duniani kote, kama vile Kongamano la kutafakari upya michakato inayohusiana na Malengo ya Milenia MDGs, Kongamano la Programu ya Vitendo la Idadi ya Watu na Maendeleo (ICDP) baada ya miaka 20, pamoja na Kongamano la Mazingira na maendeleo la Umoja wa Mataifa la Rio + 20.

Je una unaguswa na moja kati ya maeneo haya? 

Kampeni ya Vitendo Bilioni 7 itaandaa na kuhamasisha vitendo katika maeneo saba ya maendeleo: 1) umasikini na ukosefu wa usawa, 2) uwezeshwaji wa wanawake na wasichana, 3) afya ya uzazi na haki, 4) vijana, 5) Wazee, 6) mazingira na 7) ukuaji wa miji. 


Njia za kujiunga na harakati ya Vitendo Bilioni 7

Tuma habari yako kwenye www.7billionactions.org
• Kila mmoja ana nafasi ya kuifanya dunia ya watu bilioni 7 kuwa bora zaidi. Duniani kote mashirika na watu binafsi wanafanya vitendo chanya na vyenye maana. Waalimu, madaktari, wakunga, wasanii, wanablogu, maafisa wa serikali, wazazi … watu kila mahali wanachangia kwa njia binafsi, za kipekee na zenye ubunifu katika harakati ya kimataifa kwa ajili ya watu wote.
• Tupe habari yako: Je ni kwa namna gani unachukua hatua kwa vitendo kwa ajili ya watu wote?
• Kampeni ya Vitendo Bilioni 7 inalenga kukusanya habari za watu binafsi na mashirika yanayochangia mabadiliko. Habari ambazo zinaweza kuwatia moyo wengine kuchukua hatua. Unaweza pia kutupa habari kuhusu mtu unayemfahamu anayechukua hatua za kuleta mabadiliko kwenye jamii yako, iwe ni kitendo rahisi cha wema ama jitihada kubwa iliyopangwa. Pia unaweza kutafuta – na kujiunga na – watu ambao habari zao za mabadiliko zinafanana na yako.
• Nenda http://7billionactions.org/stories na tupatie habari yako

Buni tafsiri yako mwenyewe ya wimbo wa “United” – muziki wa kuhamasisha vitendo
Kampeni ya Vitendo Bilioni 7  inafanya mabadiliko chanya kupitia lugha ya kimataifa ya muziki. Muziki una nguvu ya kuvunja mipaka kati ya watu. Muziki unavuka mipaka ya umbali wa kijiografia, kisiasa, kiuchumi, kiroho na kiitikadi, na kuwaunganisha watu kila mahali kuwa jamii ya moja ya mwanadamu.
• Tuna wimbo mmoja. Tafsiri nyingi za aina yake. Na lengo moja: kuhamasisha vitendo.
• Vitendo Bilioni 7 inashirikiana na Mfuko wa Cheza kwa Ajili ya Mabadiliko, waliojitolea kuiunganisha dunia kupitia muziki. Wamebuni wimbo kwa ajili ya Vitendo Bilioni 7 unaoitwa “United.” Wanamuziki wenye vipaji duniani kote wanautafsiri kwa kutumia sauti zao tofauti, ala na mitindo ya muziki.
• Cheza kwa Ajili ya Mabadiliko itatengeneza mseto wenye tafsiri tofauti zilizotengenezwa kila sehemu duniani
• Unataka kuutia vikorombwezo upya muziki huo?
• Buni tafsiri yako ya wimbo wa “United” : http://www.7billionactions.org/music

Jiunge na shindano la filamu fupi la “1 ya Bilioni 7”
• Filamu ina nguvu ya kipekee ya kuhuisha mada na kuzipa sura ya utu changamoto zinazoikabili dunia – na utatuzi wake. “1 ya Bilioni 7” ni shindano la kimataifa la filamu fupi, lililoandaliwa na mpango bunifu wa Vitendo Bilioni 7 pamoja na Mfuko wa 10.12.48.
• Shindano hilo limekusudiwa kuwahamasisha watengenezaji wa filamu wa kila mahali kudodosa moja ya maeneo haya saba ya muhimu: 1) Umasikini na jinsi ya kuuvunja mzunguko wa ukosefu wa usawa, 2) Uwezeshwaji na maendeleo ya wanawake na wasichana, 3) Vijana, 4) Afya ya uzazi na haki,  5) Mazingira yenye afya na watu wenye afya, 6) Kuzeeka, 7) Mipango-ya-Ukuaji wa miji kwa ajili ya maongezeko.
• Masharti ya uwasilishaji:
    o Filamu ni lazima iwe katika muundo wa kidijitali.
    o Filamu ziwe na urefu wa dakika 1 mpaka 10, hiyo ni pamoja na maandishi ya sifa.
    o Iwapo Maingizo ya filamu yatawasilishwa kwa lugha nyingine maingizo hayo ni lazima yawe na maandishi ya tafsiri za mazungumzo kwa Kiingereza.
    o Mwandishi wa kazi atawajibika kwa ubunifu wa kazi.
    o Kila ingizo ni lazima lilenge moja au zaidi kati ya mada 7 muhimu
    o Kila timu au mtu binafsi anaweza kuwasilisha filamu fupi zisizozidi mbili.
    o Filamu ni lazima ziambatane na fomu ya mtandaoni ya ingizo.
• Baraza la waamuzi litachaguliwa na Vitendo Bilioni 7 pamoja na Mfuko wa 10.12.48, na litajumuisha wawakilishi kutoka kwenye jamii ya filamu, mashirika ya haki za binadamu, na watu binafsi. Baraza la waamuzi litachagua washindani kumi wa fainali kutoka kwenye maingizo yaliyowasilishwa. Baada ya hapo, kwa kupitia upigaji kura wa kwenye mtandao, watumiaji wa mtandao watachagua washindi watatu. Upigaji kura utafanyika kuanzia Februari 16 mpaka Machi 6, 2012. 
• Muda wa mwisho wa kuwasilisha maingizo utakuwa saa 3 usiku UTC/GMT tarehe 15 Februari, 2012. Washindi watatangazwa tarehe 8 Machi 2012, ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake. 
• Onesha video yako: www.7billionactions.org, www.fundacion101248.org na https://www.facebook.com/7billionactions?sk=app_154219237995139 (fomu itapatikana kuanzia tarehe 31 Oktoba, 2011).

Tupe habari ya shirika lako ili uwahamasishe wengine kuchukua hatua
• Vitendo Bilioni 7 ni wito wa kufanya kwa vitendo kwa makampuni na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.  Duniani kote, mashirika yameitikia wito huu kwa kuwaandaa wafanyakazi na washirika wao ili washiriki. Mashirika ya kila namna, katika kila eneo la dunia, yanatengeneza programu bunifu ambazo zinashughulikia masuala yanayohusiana na dunia ya watu bilioni 7.
• Tupe habari ya shirika zako: Ni kwa jinsi gani shirika lako linachukua hatua kwa ajili ya watu wote? http://www.7billionactions.org/organizations

Jiunge kwenye vyombo vya habari vya kijamii
•Tufuatilia @7billionsActions kwenye Twita: www.twitter.com/7billionactions
•    Penda Vitendo Bilioni 7 kwenye facebook: www.facebook.com/7billionactions


Nyenzo

• Blogu ya Vitendo Bilioni 7 (ili kupata habari mpya kutoka kwa timu ya Vitendo Bilioni 7)
• Kijitabu cha Maelezo mafupi
• Makaratasi ya Maelezo Rasmi
• Maelezo yanayolenga:
• Watu binafsi
• Mashirika ya umoja wa Mataifa
• Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali
• Mifuko ya Fedha
• Makampuni
• Kiolezo cha Barua
• Namna ya Kuweka Alama
• Mwongozo wa mitindo
• Nembo
• Mabango
• Video
• UNFPA
• National Geographic
• Matoleo kwa Vyombo vya Habari


Wasiliana na   

Bw. Alvaro Serrano
Meneja wa kampeni Vitendo Bilioni 7
Barua Pepe: serrano@unpfa.org
Simu: +1 212 297 5036

Bi. María F. Ruiz de Larrinaga
Mratibu wa Kampeni
Barua Pepe: larrinaga@unfpa.org
Simu: +1 212 297 4957

Bi. Nicole Carta
Sekta Binafsi na Mifuko ya Fedha
Barua Pepe: carta@unfpa.org
Simu: + 1 212 297 5242               

Bi. Nobuko Takahashi
Ubia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Barua Pepe: takahashi@unfpa.org
Simu: +1 212 297 5386

Bi. Noemi Espinoza
Ubia Umoja wa Mataifa
Barua Pepe: nespinoza@unfpa.org
Simu: +1 212 297 4939


Bi. Azza Karam
Ubia Umoja wa Mataifa
Barua Pepe: karam@unfpa.org 
Simu: +1 212 297 5255

Bi. Katja Iversen
Ubia Umoja wa Mataifa
Barua Pepe: iversen@unfpa.org
Simu: +1 917 403 3063


Bw. Omar Gharzeddine
Uhusiano na Vyombo vya Habari
Barua Pepe: gharzeddine@unfpa.org
Simu: +1 212 297-5028


Bi. Ida Jeng Christensen
Vyombo vya Habari vya Kijamii
Barua Pepe: ichristensen@unfpa.org 
Simu: +1 212 297 5006